Gazidis ameweka wazi kuwa mchakato huo utakapoanza utaongozwa na yeye mwenyewe, mkuu wa mahusiano ya soka Raul Sanllehi na Afisa mwajiri wa klabu Sven Mislintat.
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, anatajwa zaidi kuchukua nafasi ya mzee Wenger ambaye amekaa klabuni hapo kwa miaka 22. Kocha mwingine ni Carlo Ancelotti pamoja na Massimiliano Allegri ambaye ni kocha wa Juventus.
Mbali na hao imeelezwa kuwa Mkurugenzi Gazidis ana uhusiano wa karibu na nahodha wa zamani wa timu hiyo Mikel Arteta ambaye kwasasa ni msaidizi wa Pep Guardiola kwenye kikosi cha Manchester City.
Orodha hiyo haijakamilika bila jina la nyota wa zamani wa timu hiyo Thierry Henry ambaye naye anatajwa miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi ya Wenger. Makocha wengine ni kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique na kocha wa Hoffenheim Julian Nagelsmann.
No comments:
Post a Comment