Friday, April 20, 2018

SEVEN MOSHA AJIBU SHUTUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA ALIKIBA

Meneja wa msanii Alikiba, Seven Mosha amejibu madai ya yeye kuwahi kuwa katika mahusiano na muimbaji huyo.

Akizungumza jana mjini Mombasa amesema hilo halina ukweli na ni dhana potofu iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuwa ni vigumu kwa mwanamke kufanya kazi na mwanaume kwa uweledi.

“Unajua kama mwanamke unapofanya kazi na mwanaume inakuwa ni vigumu kwa jamiii kukubali kwamba unaweza kufanya kazi yake professional, ni vitu ambavyo tunatengemea kwenye entertainment vinatokea, kwa hiyo yeah! (anapuuzia),” amesema Seven.

Katika hatua nyingine amezungumzia sherehe ya Alikiba itanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam kwa kueleza kuwa shughuli hiyo ni April 29, 2018, hata hivyo hakutaka kuweka wazi ni wapi hasa itafanyika.

No comments:

Post a Comment