Friday, April 20, 2018

COMEY: HAKUNA KIONGOZI ANAYEWEZA KUMBADILI TABIA RAIS TRUMP

Aliyekuwa mkuu wa FBI nchini Marekani, James Comey ameiambia BBC kuwa haamini kuna kiongozi yoyote wa karibu na Rais wa Marekani Donald Trump anaweza kumbadilisha tabia yake,
Anasema tabia zake zinahatarisha hadhi ya nchi.

Kabla ya kufukuzwa na Trump Comey aliongoza uchunguzi dhidi ya kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Akizungumza katika kipindi cha Newsnight Comey anasema tabia za Trump zinaathiri wale wanaomzunguka.

"Nadhani tabia yake inaathiri hasa hasa kwenye suala la ukweli na jambo la msingi ni jinsi tabia hizo zinavyoathiri taasisi na watu wa karibu wake.Ana tabia a kuongea uongo na kuwa lazimisha wale wanamuunga mkono kukubalina naye na kuamini"

Trump alimshutumu Comey kuwa anayoyazungumza na uongo na siasa zake za ubaguzi.

No comments:

Post a Comment