Wednesday, April 25, 2018

NSAJIGWA ASEMA WAPO IMARA KUVAANA NA SIMBA

YANGA ipo mkoani Morogoro ikiendelea kujifua na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wao wa jadi Sim­ba huku wachezaji wake nyota wakiingia kambini mkoani humo kujiandaa na mchezo huo.

Timu hiyo imeweka kambi Morogoro ikitokea Mbeya ili­pocheza mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City na kutoka sare ya bao 1-1.

Simba na Yanga zinatara­jiwa kuvaana Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na kikosi chao kipo imara kuvaana na Simba.

Nsajigwa alisema, tayari wachezaji wao waliokuwa na majeraha ambao ni Papy Kabamba Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Ibrahim Ajibu na Andrew Vicent ‘Dante’ wameanza mazoezi.

Aliwataja mabeki Kelvin Yondani na Hassani Kessy waliokuwa na kadi tatu za njano nao wamejiunga na kambi hiyo ya siku sita kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba.

“Kambi yetu inaendelea vizuri na kikubwa tunafura­hia kuona wachezaji wetu waliokuwa na majeraha wameripoti kambini tulio­waacha Dar baada ya sisi kwenda Mbeya tulipocheza na Mbeya City.

“Hivyo, baada ya kuripoti wachezaji hao wameendelea na program za mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo muhimu ambao tunahi­taji pointi tatu.

“Kikubwa tulichokipanga hivi sasa ni kushinda mechi zote zilizokuwa mbele yetu ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa tunaoutetea, kama unavyojua wapinzani wetu Simba wanaongoza ligi.

“Niwaambie Wanayanga kuungana kwa pamoja kupambana ili tufanikishe malengo yetu ya ubingwa kwani bado ligi mbichi kuto­kana na idadi ya michezo tuliyoibakisha,” alisema Nsajigwa.

Wakati huohuo, beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kes­sy ametamka kuwa binafsi yeye yupo fiti na tayari kwa ajili ya mechi ya watani wa jadi, Simba, hivyo waje tu.

Kessy alisema, hakuna mchezaji mgeni kwake Simba anayemuhofia, kwani wote wachezaji wa kawa­ida wenye viwango sawa ambao Yanga wapo.

“Binafsi sijaumbwa na uwoga nikiwa na maana kuwa wapo baadhi ya wachezaji zinapofikia mechi hizi za ‘derby’ wanakuwa na hofu kubwa, lakini kwangu wala sina hofu, nipo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

Katika ligi kuu, Simba ina pointi 59 kileleni ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 48. Hata hivyo, Yanga ina mich­ezo miwili zaidi.

No comments:

Post a Comment