Wednesday, May 3, 2017

WATU WATATU WAHOFIWA KUFA KUTOKANA NA AJALI YA LORI NA DALADALA


Dar es Salaam. Wanafunzi watatu wanahofiwa kufa katika ajali iliyotokea Barabara ya Nyerere jijini hapa ikihusisha lori na daladala.

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea asubuhi hii eneo la Quality Centre ikihusisha daladala linalofanya safari kati ya Gongo la Mboto na Msasani.

Taarifa iliyotangazwa na Kituo cha Radio Clouds FM inasema kutokana na ajali hiyo, kumekuwa na msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.

No comments:

Post a Comment