Thursday, April 5, 2018

ALIYEKUWA RAIS WA BRAZIL LULA DA SILVA KUFUNGWA MIAKA 12 JELA

Mahakama ya rufaa nchini Brazil imeagiza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na miwili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi.

Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.

Hatia hiyo imetokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ''Operation Car Wash''

Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki saba na tisini.

Lula da silva amekua akitarajiwa na watu wengi kusimama kama mgombea asie na ushindani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi octoba,

Lakini ndoto hizo zimeisha baada ya mahakama kuu kuamuru mwanasiasa huyo mkongwe aanze kifungo cha miaka 12 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya ufisaidi.

Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali, waandamanaji katika mji wa Sao Bernardo wanataka Da silva aachiwe huru, " mkusanyiko wetu wa leo ni kuhakikisha kuwa rais wetu wa zamani Lula, ana haki ya kurudi kuwa mgombea wa Urais na kama kweli hawataki kumuona basi njia pekee ni kumshinda katika uchaguzo''

Baadhi ya watu wanapinga kuachiwa huru kwa Lula Da Silva na badala yake jeshi ndio liongoze nchi hiyo, ''Kama mahakama kuu haitamuweka Lula jela, basi tunataka jeshi ndio lishike madaraka kwasababu taasisi zimejaa rushwa , zote hadi mahakama''

Mbali na kukutwa na hatia Lula amekua akipinga vikali kuhusika na kashfa yoyote ya rushwa anasema kuwa amekua akipinga vikali uonevu wa aina yoyote hivyo hatakubali uonevu wa mahakama.
Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 72 atabaki uraiani kwa muda hadi pale nyaraka za kifungo chake zitakapo kamilika.

Lula Da silva amekua madaraki kati yam waka 2003 hadi 2011. Kama angeingia kama mgombea katika uchaguzi wa mwezi oktoba huenda angeshinda kwa kishindo kutokana na umaarufu wake.


No comments:

Post a Comment