Wednesday, March 14, 2018

UN WAINGIA MAKUBALIANO NA SERIKALI KUTANGAZA MPANGO WA MAENDELEO

UMOJA wa Mataifa umeingia makubaliano ya kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa habari za maendeleo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO).

Makubaliano hayo yamelenga kuimarisha upatikanaji na utoaji habari wa pamoja kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa serikali na malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.

Kwa mujibu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez  makubaliano hayo yatachagiza kupatikana kwa habari kuhusiana na utekelezaji  wa malengo ya maendeleo endelevu unaokwenda sambamba na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa Tanzania.

Akizungumzia malengo hayo kwa maofisa wa mawasiliano wa serikali wanaokutana mjini Arusha kwa semina ya wiki moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya TAGCO na Wizara ya Habari na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa, alisisitiza kuwa malengo hayo yanahitaji kuwasilishwa kwa wananchi na pia kupigiwa chapuo.

No comments:

Post a Comment