Kikosi cha Simba kikiwa kimeondoka nchini kuelekea Masry kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry, kocha wa Mbao Etienne Ndayiragije amesema kila kitu kinawezekana kwenye soka na Simba inaweza kupata matokeo ikiwa ugenini.
Simba itacheza mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry ugenini baada ya kutoka sare ya kufungana 2-2 kwenye mechi ya awali iliochezwa uwanja wa taifa.
“Kilakitu kinawezekana kwenye football, walicheza dakika 90 nyumbani wanakwenda kucheza nyingine ugenini, uwanja ni uleule pitch ni ileile ni jinsi gani wamejipanga Mungu akiwajalia kila kitu kinawezekana.”
“Wanatakiwa kujua hii siyo ligi ni mechi za mtoano, ukiwa ugenini kama unajiaandaa na hizi mechi za Caf unatakiwa kushambulia kwa sababu hauna haja ya kujilinda. Nikiangalia aina ya wachezaji ambao Simba inao wanauzoefu wa kufunga wakipata nafasi watafunga.”
“Wakijiandaa kwa ajili ya kujilinda sijui itakuwaje itategemea na namna ambavyo mwalimu ame-plan.”
Kocha huyo amesema, kiufundi mechi za aina hiyo zinategemea mambo mengi sana nje na ndani ya uwanja ambayo yanaweza kuleta ushindi au kinyume chake.
“Mechi kama hizi zinatemea na jinsi mtakavyosafiri, watafika lini, watafikia wapi, hali ya hewa ilivyo, nayo huwa inachangia kwa asilimia kubwa.”
Kama unakumbuka Mbao ikiwa chini ya Etiene ilicheza na Simba fainali ya FA Cup na kupoteza mchezo huo kwa mufungwa 2-1 Simba wakabeba ndoo iliyowapa tiketi ya mucheza Caf Confederation Cup, endapo Mbao wangeshinda mechi hiyo wangekuwa wawakilishi wa nchi katika michuano ya Afrika.
Etiene amesema endapo Mbao ingekuwa inashiriki mashindano ya kimataifa anadhani ingepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau nchini hivyo wangesajili na kufanya maandalizi ya kutosha, uzoefu wake kwenye mashindano ya kimataifa ungeisaidia timu.
“Kwanza ikitokea umepata nafasi ya kushiriki matokeo yanatokana na maandalizi. Ingekuwa ni Mbao ndio inawakilisha Tanzania naimani kuwa uongozi wa timu, mkoa hadi nchi ungesapoti sana maandalizi si dhani kama kina Buswita na wengine wangeondoka kwenye klabu.”
“Wangepatikana wadhamini tungesajili na kujiandaa na maandalizi yasingekuwa kama ilivyo sasa hivi. Najua kwa sababu nimeshashiriki kombe la shirikisho nikiwa kocha Vital ‘O na Ngaya Club najua nini kinahitajika kwa hiyo ningejiandaa. Zote nilizifikisha mechi za mwisho kabla ya makundi.”
Kuhusu mapungufu aliyoyaona kwa Al Masry ambayo Simba wanaweza kuyatumia ikawa faida kwao, kocha huyo amesema kila timu ina mapungufu na uwezo wake lakini pia inategemea plan za kocha kwa mchezo husika.
“Katika mpira kila timu inakuwa na mapungufu yake lakini inakuwa na uwezo wake pia, hizi ni mechi ambazo unatakiwa kucheza kitimu (mwalimu ndio anatoa plan ya mechi). Kutokana na mechi anajua atalinda wapi, niwasubiri katikati, niwafuate kwao au niwasubiri kwetu hayo ni maamuzi ya kocha kulingana na alivyouona mchezo.”

No comments:
Post a Comment