SERIKALI imesema iko mbioni kukamilisha mchakato wa kuunda bodi mpya na menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) baada ya iliyokuwapo kuvunjwa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ndiye aliyetoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akijibu hoja zilizoibuka wakati wa makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.
Alisema tayari serikali imeshapata watu wa kuingia kwenye uongozi wa shirika hilo na kinachofanyika sasa ni mchujo wa majina yaliyopendekezwa.
Waziri huyo pia aliuagiza uongozi wa NHC kukutana na chama cha wapangaji ili kutatua mgogoro uliopo baina yao.
Juzi wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, mjumbe wa kamati hiyo, Halima Bulembo, aliitaka serikali kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro wa kiuongozi uliopo NHC ikiwa ni pamoja na kuteua bodi na menejimenti ya shirika.
Bulembo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), pia alisema kumekuwapo taarifa kwamba NHC inaelekea kufilisika kutokana na kuwa na madeni makubwa kuliko mali zake.
Alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo, kamati yao iliagiza kuwasilishwa mbele yake taarifa kuhusu hali ya maendeleo ya utendaji wa shirika hilo.
Bulembo alisema wizara iliwasilisha taarifa hiyo mbele ya kamati yao na walipoijadili kwa kina, walibaini kutokuwapo kwa bodi na menejimenti ya NHC kunadhoofisha utendaji wa shirika.
Alisema kamati yao pia imeridhishwa na taarifa ya ukaguzi wa shirika uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayotoa taswira halisi ya hali ya shirika kuliko taarifa zilizokuwa zimesambaa.
"Hata hivyo, kamati inaishauri serikali kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro wa kiuongozi uliopo katika shirika ikiwa ni pamoja na kuteua bodi na menejimenti ya shirika," alisema Bulembo na kuongeza:
"Pia ikamilishe tathmini ya hali ya ukwasi wa shirika ili liruhusiwe kuendelea kukopa kwa ajii ya kuendelea na miradi yake.
"Serikali pia ikamilishe Sera ya Taifa ya Nyumba na kutekeleza ahadi yake ya kukutana na wapangaji wa NHC wa muda mrefu hasa wastaafu ili kumaliza mgogoro wa upangishaji wao."

No comments:
Post a Comment