Familia ya mwanafunzi wa kwanza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), anayedaiwa kuuawa na polisi wiki iliyopita, Aquilina Akwilini imekabidhi serikali bajeti ya maziko ya zaidi ya Sh milioni 80.
Msemaji wa Familia, Festo Kavishe amekabidhi bajeti hiyo leo Jumanne Februari 20, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwipalo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisali Makori leo. "Hayo ndiyo makubaliano ya familia, tumewakabidhi wataenda na kujadiliana kisha tutakutana nao saa 10 jioni leo, kisha watatueleza ya kwao pia, tunachohitaji ndugu yetu apumzike kwa amani," amesema Kavishe.
Marehemu Aquilina ambaye aliuawa kwa risasi Ijumaa iliyopita akiwa katika basi baada ya polisi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliokuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Wilaya ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao, anatarajiwa kuagwa Alhamisi wiki hii katika viwanja vya NIT na kusafirishwa Rombo mkoani Kilimanjaro, Ijumaa.
No comments:
Post a Comment