JB;SIMFAHAMU NAY WA MITEGO
Msanii Jacob Steven JB' amedai kutomfahamu Nay wa Mitego na kusema
pamoja na kusikia sehemu mbali mbali za maneno ya kashfa kutoka kwa
msanii huyo yeye bado anampenda japokuwa hamjui na wala hajawahi
kusikiliza nyimbo zake.
Akilijibu swali la Mtangazaji wa eNewz Duwe Santana kuhusu jinsi
alivyopokea kauli ya wasanii waliondamana kuitwa 'Matahira' JB amesema
hajaisikia kauli hiyo na wala hamtambui msanii huyo hivyo yeye
anamuachia tu Mungu.
"Mwalimu wangu wa economic aliwahi kuniambia One man's meat could be
another man poison, kwahiyo kama wao wametuona sisi matahira sisi
tunawashukuru sana. Mimi ni Mkristo sijafunzwa kutukana nimefunzwa
kuwapenda watu wote na kuwaheshimu"- JB alianza kufunguka
No comments:
Post a Comment