WAZIRI
wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini
kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa
madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma
chakavu.
Dk
Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita,
madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye
utaratibu wa kuwapeleka mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa
madogo wazitatue haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.
“Wapeni
masomo wamekosea wapi, walekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini
tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake
tunao, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya
mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu
Alisema
kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama
barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki
katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi
hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
No comments:
Post a Comment