Zipo dalili za awali ambazo huonekana kwa mtu mwenye virusi vya ukimwi, na dalili hizo awali ni kama ifuatavyo;
- Homa
- Kusikia baridi
- Maumivu ya joints
- Maumivu ya misuli
- Koo kavu
- Jasho (Hasa usiku)
- Uchovu wa mwili
- Udhaifu
- Kukonda
Baada ya dalili hizi za awali kutoweka, mara nyingi hakuna dalili zo
zote zitakazooneka kwa kipindi kirefu. Wakati huu wadudu hawa wanazidi
kuzaliana, kuongezeka na kuharibu mfumo wa kinga za mwili. Kipindi hiki
cha ukimya kinaweza kwenda hadi miaka 3 wakati huu wote mtu akijisikia
vizuri tu na kuonekana mwenye afya.
Na ndio maana mara nyingi watu hushauriwa kupima virusi vya ukimwi kila baada ya mwezi ili kujua kama atakuwa ameambukizwa.
Baada ya kuona dalili za awali sasa naomba tuangalie dalili mwisho za ugonjwa huu.
Dalili za mwisho za UKIMWI zinaweza kuwa:
- Kutoona vizuri.
- Kuharisha mfululizo.
- Kikohozi kikavu.
- Homa kali inayokwenda kwa muda mrefu.
- Kuvuja jasho usiku.
- Uchovu wa mwili mfululizo.
- Kupumua kwa shida.
- Kukonda.
- Vijidoa vyeupe kwende midomo na ulimi.
Hivyo kila wakati hakikisha unakwenda kwenye vituo vya afya ili Kupata ushauri lakini pia kupima kama una mambukizi ya virusi vyaUKIMWI.
Kwa leo naomba niishie hapa naomba uendelee kutembelea mtandao huu wa ADACOMPLANET BLOG kila wakati
No comments:
Post a Comment