Tuesday, September 5, 2017

MASHABIKI WALALAMIKA MECHI YA SIMBA NA AZAM KUPELEKWA AZAM COMPLEX

Mashabiki wa soka wamelalamika kitendo cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC kupelekwa Azam Complex, Chamazi.


TFF imeamua kutangaza michezo ya Simba na Yanga dhidi ya Azam FC, sasa nayo itakuwa inachezwa Azam Complex tofauti na awali kutokana na ukubwa wake ilitakiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa au ule wa Uhuru.

Safari hii, Azam FC itaikaribisha Simba Chamazi katika mechi itakayopigwa Jumamosi ikiwa ni ya pili ya Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kila timu.

Mashabiki hao walioandika maoni katika mitandao ya Kijamii ya Salehjembe pamoja na blog yenye ya Salehjembe wamelia kutotendewa haki.

Kwa ujumla mashabiki hao wamelalamika kuhusiana na udogo wa uwanja wa Azam Complex wenye uwezo wa kuchukua watu 7,000.

“Nafikiri hii si sawa, wote tunajua uwanja huo ni mdogo na hii ni mechi kubwa. Wanatunyima haki ya kuona mechi hiyo.

“Angalau kungekuwa hakuna viwanja, lakini kuna Uhuru upo pale.”

Wengine walilalamikia umbali wa Chamazi na muda ambao mechi imepangwa Saa 1 usiku.

Lakini Azam FC imekuwa na kilio cha kutaka kucheza mechi zake nyumbani jambo ambalo hatimaye limetimia.

No comments:

Post a Comment