Tuesday, September 5, 2017

MSHAMBULIAJI DELE ALLI ANASWA NA KAMERA AKIMUONYESHA REFA KIDOLE CHA KATI

Mshambuliaji wa Tottenham, Dele Alli amenaswa na kamera za uwanjani akimuonyesha mwamuzi kidole cha kati wakati wa mechi ya England na Slovakia, huku akiomba radhi kwenye mtandao wake wa Twitter kutokana na tafsiri iliyochukuliwa.

Mechi hiyo iliisha kwa England kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ikiwa ni mashindano ya kimataifa ya kufuzu Kombe la Dunia mwakani.

Mchezaji huyo alikanusha jambo na kusema kuwa hakudhamiria kumuonyesha refa huyo bali alilenga kufanya utani na mchezaji mwenzake  Kyle Walker.

No comments:

Post a Comment