Tuesday, September 5, 2017

MAAFISA WA POLISI 92 WALAZWA WAKIHOFIWA KINDUPINDU


Maafisa 92 wa polisi nchini Kenya wamelazwa hospitalini Nairobi na viunga vyake wakihofiwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu, wizara ya afya nchini humo imesema.
Maafisa hao wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Kenyatta, hospitali ya Sinai na katika hospitali ya wanawake ya Nairobi Women’s.

“Polisi hao inashukiwa waliambukizwa kipindupindu katika mgahawa wa polisi katika eneo la Nairobi Area,” taarifa ya wizara hiyo imesema.

Mgahawa huo umefungwa kwa muda usiojulikana huku uchunguzi ukiendelea.

Waziri Cleophas Mailu amesema maafisa hao wanaendelea kupata nafuu hospitalini.

Gazeti la kibinafsi la the Star linaweza baadhi ya maafisa walikuwa kazini wakati wa kutangazwa kwa uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

Gavana wa Nairobi Mike Sonke alikuwa Jumapili ametoa taarifa na kusema hali imethibitiwa.
Alisema hatua zimechukuliwa “kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.”

No comments:

Post a Comment