Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionesha waandishi wa habari baadhi ya silaha zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro. |
Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupata jumla ya bunduki kumi za
aina nne tofauti zikiwemo Sub-Machine Gun sita baada ya operesheni ya
wiki mbili iliyoanza tarehe 15.02.2017 katika wilaya ya Ngorongoro.
Silaha mbalimbali zikiwemo SMG 6 pamoja na risasi 59 zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika katika wilaya ya Ngorongoro. |
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi, Kamanda wa
Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema silaha
hizo zilipatikana katika vijiji vya Olorieni Magaiduru, Oldonyosambu na
Sale vilivyopo katika tarafa za Loliondo na Sale.
Alisema mafanikio hayo yalitokana na taarifa fiche ambazo zilibainisha
kwamba kuna baadhi ya watu wanamiliki silaha za kivita hivyo mahojiano
makali baina ya askari wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa Kimila na
kuwataka wasalimishe silaha popote pale ambapo walikuwa wanaamini kwamba
silaha hizo zitawafikia Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment