Friday, February 10, 2017

MASHABIKI WA STAND UNITED WANAOKATA TAMAA ,KOCHA AMEWAPA NENO


Stand United inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Majimaji kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, kocha wa Stand Augustino Malindi amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Tumejipanga kushinda mechi dhidi ya Majimaji, mimi nafikiri kwenye mpira huwa hakuna sababu kwamba kwa nini umepoteza inapofikia wakati unafungwa inabidi ukubali na inapotokea timu imeshinda ni sawa kwa sababu ndio mpira ulivyo ndio maana timu inafanya mazoezi.” – Augustino Malindi

“Kuna sababu nyingine ambazo hata ukiziongelea inakuwa sio, mechi yetu tuliyocheza Kagera mwamuzi hakuwa fair kwa upande wetu kwa sababu tulipata penati mbili lakini hatukupewa hali kadhalika fourth official akamtoa kocha wetu wa makipa na kuwapandisha jukwaani.”

“Tumeenda Tanga hali ikawa hivyohivyo, mechi ambazo tulikuwa tunaweza kushinda lakini tunashindwa kutokana na maamuzi ya ma-referee.”

“Mashabiki wetu wasikate tama, watupe sapoti kama walivyotupokea tulivyorudi kucheza na Yanga. Mwalimu amefanyia kazi safu ya ushambuliaji na ulinzi tunaingia kucheza na Majimaji tukiamini tutapata ushindi na kuibuka na pointi tatu.”

No comments:

Post a Comment