Polis wanajikakamua kutatua visa hivyo ambayo vinawaacha wanawake na mshutuko mkubwa.
"Kulikuwa na mwanga mkali uliosababisha nipoteze fahamu. Saa moja baadaye niligundua kuwa nywele pia ikuwa imekatwa," alisema Sunita Devi, mwamamke mwenye umri wa miak 53 kutoka Haryana.
"Nemeshindwa kulala wala kufanya chochote. Nilisoma kuhusu visa hivi vikifanyika huko Rajasthan, lakini sikufikiria kingetendeka kwangu," aliongeza.
Mbali kidogo mwanamke mwingine Asha Devi naee alipoteza nywele yake katika shambulizi kama hilo siku iliyofuata.
Lakini wakati huo mshambuliaji aliripotiwa kuwa mwanamke, Baba mkwe wake Asha Devi, Suraj Pal anasema kuwa kufuaia kisa hicho, alimshauri pamoja na wanawake wengine wa familia kuhamia nyumba ya jamaa wao kati jimbo la Uttar Pradesh.
Bwana Pal anasema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi alitoka nje kufanya kazi zake, "Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaid ya dakika 30. Tulipata amapoteza fahamu katika chumba cha kuoga. Nyele yake ilikuwa imekatwa na kutupwa sakafuni."alisema.
Ripoti za kunyolewa wanawake kwanza ziliibuka mapema Julai kutoka jimbo la Rajasthan, lakini visa sawa na hivyo kwa sasa vinaripotiwa kutoka Haryan na hata mji mkuu Delhi.
Sunita Devi anaishi katika jamii ya wafanya biashara na wakulima, Baadhi wa majirani zake wanachukua zamu kukaa naye hadi apate kuondokewa na mshutuko.
Anasema mshambuliaji wake alikuwa ni mwanamume mzee ambaye alikuwa amevaa nguo nyeupe.
No comments:
Post a Comment