Timu gani itasonga mbele kwa kuingia hatua ya Robo Fainali ya Kombe la
Shirikisho kati ya Young Africans na Kiluvya United? Majibu ya swali
hilo yatapatikana leo baada ya mchezo kati ya timu hizo utakaofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Huu ni mchezo wa kukamilisha raundi ya sita ambayo ilikutanisha timu 16
Bora na inayofanya vema huingia hatua Nane Bora au Robo Fainali.
Mshindi kati ya timu hizo, itaungana na timu nyingine saba
zilizotangulia kucheza Robo Fainali ambazo ni Simba na Azam FC za Dar es
Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha,
Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50
milioni. Bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye
michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi
Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi
ya Mabingwa Afrika.
No comments:
Post a Comment