Liverpool wamekataa ombi la Barcelona la kutaka kumnunua mchezaji raia wa Brazil Philippe Coutinho kwa kima cha pauni milioni 90.
Hili ndilo ombi la pili kutolewa na Barcelona baada ya lile la kwanza la pauni milioni 72 kukataliwa.
Liverpool wamesisitiza kuwa Coutinho ambaye alijiunga nao kutoka Inter Milan mwaka 2013 kwa pauni milioni 8.5 hauzwi.
Barcelona walimuuza mshambuliaji wake Neymar kwenda St-Germain kwa kima cha pauni milioni 200 wiki iliyopita.
Coutinho ambaye alifunga mabao 14 msimu uliopita alikaa muda wa wiki sita kutokana na jeraha, alisaini mkataba wa miaka mitano mwezi Januari.
No comments:
Post a Comment