Thursday, August 10, 2017

MANJI AENDELEA KUSOTA MAHAKAMANI


Kesi inayomkabili mfanyabiashara na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, imeahirishwa leo hadi Agosti 22 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi, Cyprian Mkehe.

Maelezo hayo yalisomwa na wakili wa serikali, Timon Vitalis, yalihusu utambulisho wa jina lake kamili, kazi anayofanya, tarehe aliyokamatwa, alivyopelekwa kwa mkemia na alivyopekuliwa nyumbani kwake. Katika kesi hiyo Manji anawakilishwa na wakili Alex Mgongolwa.

No comments:

Post a Comment