Wednesday, August 9, 2017

BILIONI BILL GATES AIBUKIA KIJIJINI TANGA



William Henry Gates III maarufu kama Bill Gates na Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft iliyomfanya kuwa mtu tajiri namba moja  duniani na mwanzilishi wa mashirika lukuki yasiyo ya kiserikali yenye kusaidia jamii yupo nchini.

Jana  ametembelea kijiji cha Kicheba wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga kwa lengo la kuangalia maswala mbalimbali ya afya ikiwemo utumiaji wa dawa za mabusha, matende ili kuangalia ni namna gani anaweza kusaidia kwenye sekta hiyo ya Afya.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo (kushoto) akiwa na Bill Gatesbpamoja na mmoja wa viongozi wa kinamama wa wilaya hiyo katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga jana
Bill Gates akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wilaya ya Muheza akiwamo Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo na Mbunge Mhe Adadi Rajabu (wa nne kulia) katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga jana

No comments:

Post a Comment