Klabu ya Yanga imesafisha hali ya hewa kutokana na taarifa
zinazovumishwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuachwa kwa baadhi ya
wachezaji itakapofika mwishoni mwa msimu huu kutokana na matatizo ya
kiuchumi kwenye klabu hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu Yanga, Charles Boniface Mkwasa imeeleza kuwa, hakuna ukweli wowote wa taarifa za kuachwa kwa wachezaji, na huenda zina malengo ya kuanza kuwavuruga katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu.
“Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa . Uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi lao la ufundi. Hatujakaa kulijadili hilo wala kulifikiria bali tupo makini kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu.”
“Mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji klabuni kwetu ni kocha mkuu Mr George Lwandamina na timu yake sio kiongozi mwingine yoyote na kocha huyo hajatoa taarifa yoyote ya kumwacha mchezaji gani au yupi kumuongezea mkataba zaidi ya kila siku kuukazania uongozi kuboresha masilahi yao kwa sababu kama kocha mkuu anajivunia na kujali kazi ya vijana wake.” Imeeleza taarifa ya Katibu mkuu wa Klabu ya Yanga,Ndg Mkwasa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wachezaji wote ni muhimu na uongozi wa Yanga unajivunia kwa moyo wao thabiti kuitumikia klabu. Hivyo wamewaomba wachezaji kuwapuuza watoa habari feki za klabu, na badala yake waendelee kucheza kwa bidii.
Klabu ya Yanga ipo kambini mkoani Geita ambako jana iliibuka na ushindi wa goli 5-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Buseresere,Na hii ni salamu tosha kwa maafande wa Tanzania Prisons ambao watavaana nao Jumamosi ya wikiendi hii kunako dimba la taifa.
Timu hiyo, ilipata ushindi huo katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Waja uliopo Mkoani Geita.

No comments:
Post a Comment