KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, amesema kuwa hakuna namna ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inashuka kwenye Uwanja wa huo wa Taifa kujaribu kuendelea kukoleza mbio zao za kutwaa ubingwa msimu huu.
Akizungumza na Nipashe jana, Lwandamina, alisema kuwa michezo mitatu ya ligi kuu iliyobakia ina umuhimu mkubwa katika harakati zao za kutwaa ubingwa.
"Kila mmoja anafahamu hatua tuliyofikia sasa hakuna masihara, nashukuru wachezaji wangu wanafahamu hivyo na wameongeza umakini katika michezo iliyobakia na tutaendelea kufanya hivyo kwenye mchezo wa kesho (leo)," alisema Lwandamina.
Alisema anafahamu mchezo wa leo utakuwa mgumu kwa kuwa Mbeya City nao wanasaka ushindi.
"Sitegemei kufanya mabadiliko kwenye kikosi, ni umakini na kujituma ndicho nataka wachezaji wangu waongeze, tunahitaji ushindi," aliongezea kusema Lwandamina.
Endapo Yanga itafanikiwa kupata ushindi itakuwa imejisogeza karibu kabisa na ubingwa kwa kuwa itakuwa imefikisha pointi 65 huku ikiwa na michezo miwili mkononi.
"Kila kitu kipo wazi, kama tutashinda michezo yetu yote tutakuwa mabingwa bila kuangalia matokeo ya wenzetu hivyo akili na mawazo yetu tunayaweka kwenye michezo yetu iliyobakia," aliongezea kusema Lwandamina.
Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri, aliiambia Nipashe juzi kuwa wanafahamu ugumu wa mchezo wa leo lakini watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

No comments:
Post a Comment