Vee
Money ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Duasi’ alioshirikishwa na
Legendary Beatz ametumia mtandao wa Twitter kuyatoa ya moyoni dhidi ya
kigogo huyo, ingawa hakuweka wazi jina lake.
“Inasikitisha
kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha
jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” inasomeka tweet ya kwanza ya Vee Money.
Hata
hivyo, mwimbaji huyo ameamua kuweka heshima yake mbele na kujiepusha na
majibishano kwani kufanya hivyo anaamini kutakuwa utovu wa nidhamu.
No comments:
Post a Comment