Rais
Magufuli aliufungulia wimbo huo baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na kumtaka rapa, Nay wa Mitego
kuongeza baadhi ya maneno katika wimbo huo ili uwaguse watu wengi
zaidi.
Nay wa Mitego amedai remix ya wimbo huo iko tayari na ameongeza vitu vingi ndani ya wimbo huo.
“Kusema kweli wimbo wa Mh Rais umekamilika na muda wowote unaweza kutoka.
“Nimeongeza
mambo mengi ndani yake, kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili
ya moto mwingine kwa sababu bado ‘Wopo’ yenyewe inaendelea kufanya
vizuri,”
Rapa huyo amedai hawezi kusema ni lini project hiyo itatoka.
Katika
hatua nyingine rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea
kumuunga mkono katika muziki wake pamoja na kujitokeza kwa wingi katika
tour yake ya ‘Wapo’ ambayo imeingia ndani ya jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment