Mbunge
wa Tarime Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
John Heche ameshindwa kuendelea kuhudhuria vikao vya Bunge
vinavyoendelea mjini hapa, kutokana na matatizo ya kiafya na kulazimika
kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es
Salaam.
Heche
alipata tatizo la afya na kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Dodoma jana alfajiri. Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa
Hospitali hiyo, Dk Caroline Damian alikiri kuwa Heche, alipokewa
hospitalini hapo alfajiri ya jana na kuhudumiwa kwa muda kabla
hajasafirishwa kupelekwa mahali ambako hakuwa tayari kupataja.
“Hatujampa
rufaa ila matibabu yake yanaratibiwa na Kliniki ya Bunge, hivyo
tulimpokea na kumhudumia kwa muda kabla taratibu za kumsafirisha
hazijakamilika, tulipoambiwa ndege ya kumsafirisha ipo tayari,
aliondolewa kwetu na kusafirishwa kwa ajili ya matibabu,” alieleza daktari huyo.
Awali,
mbunge huyo alipata tatizo la afya na kulazimika kuwa chini ya
uangalizi wa kitabibu. Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar,
Salum Mwalimu, alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akijibu
maswali ya wananchi walihoji hali ya mbunge huyo, ambaye ilikuwa
ikielezwa kuwa hospitalini.
Kabla
ya muda huo kuwadia, ilielezwa kuwa Heche alipata maumivu ya tumbo
kabla hajapelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili ambako
alifanyiwa upasuaji.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema Taifa,
Tumaini Makene jana alithibitisha taarifa ya kuugua ghafla kwa Heche na
kuletwa jijini Dar es Salaam katika hospitali hiyo.
“Ni
kweli Heche aliugua ghafla akiwa Bungeni huko Dodoma, alisafirishwa kwa
ndege jana asubuhi saa moja na kuletwa Muhimbili ambako anaendelea na
matibabu,” alisema Makene.
Ofisa
Habari wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha kupokelewa Heche jana
saa nne asubuhi na kwamba anaendelea na vipimo kubaini nini tatizo
lake.
No comments:
Post a Comment