Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara.
Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara ameanza majigambo yake mapya kwa kuwaambia Mbao FC watatumia dakika tisa tu kuwaangamiza katika fainali za Kombe la FA zinazotarajiwa kuchezwa Mei 28, uwanjwa wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Manara amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Istagram kwa kujigamba kuwa Simba wanawajua vizuri Mbao FC huku akidai walishawahi kuwafunga hapo awali katika uwanja wao wa nyumbani CCM Kirumba ndani ya dakika tisa tu.
"Kama Simba ili wachukua dakika tisa kuwafunga wababe wa Gongowazi (Yanga) pale kwao Kirumba, unadhani itatuchukua dakika ngapi katika mji wenye 'Fans' wengi zaidi wa Simba kumgalagaza 'Ngariba' wao, tutashinda kokote InshaAllah". Aliandika Manara kupitia Instagram yake
Kwa upande mwingine, timu itakayoweza kuibuka kidedea kwa ushindi dhidi ya mwenzake itaweza kupatiwa kitita cha Milioni 50 fedha taslimu za kitanzania kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo pamoja na kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika linalosimamiwa na CAF.
No comments:
Post a Comment