Nafasi
hiyo imetangazwa baada ya kifo mbunge aliyekuwa anashikilia wadhifa
huo, Dk Elly Macha kufariki dunia Machi 31, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana (Jumanne) na Mwenyekiti wa NEC,
Jaji Semistocles Kaijage ni kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amemjulisha kuwepo kwa nafasi hiyo.
“Kutokana
na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza
nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na
kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya
343,”amesema.
No comments:
Post a Comment