Monday, May 28, 2018

BALE AFUNGUKA HASTAHILI KUWEKWA BENCHI

STAA wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mab­ingwa Ulaya iliyopigwa juzi, Gareth Bale, amesema al­ihuzunika kuanzia benchi ka­tika mchezo huo, akasisitiza anadhani hastahili kuwekwa benchi.

Bale aliingia kwenye mchezo huo dhidi ya Liverpool kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 nchini Ukraine, bao lake la kwanza linaweza kuingia kwenye orodha ya mabao bora katika historia ya michuano hiyo.

Bale amekuwa hana nafasi ya kudumu kwenye timu hiyo, lakini amesema kuwa sasa anataka kuwa anacheza kila wiki.

Raia huyo wa Wales, amese­ma anachokitaka Madrid hadi sasa hajakipata kwa kuwa pamoja na kupata makombe lakini anataka kucheza pia.

“Nataka kucheza kila wiki, jambo hilo halijatokea ndiyo maana nimekaa na wakala wangu tumekubaliana.

“Nafikiri natakiwa kukaa na uongozi wa timu hii ku­fahamu kuhusu mustakab­ali wangu, kila wiki nataka kucheza lakini jambo hilo halijatokea kwangu msimu huu.

“Nimekaa nje kama wiki sita nikiwa mgonjwa, lakini baada ya hapo nimekuwa fiti na kutamani sana kucheza.

“Nimesikitika kwa kuwa sikuanza kwenye mchezo huu, lakini naamini kuwa anayeamua ni kocha na jambo zuri kwangu ni kwa kuwa nimeingia na kufanya makubwa,” alisema Bale.

No comments:

Post a Comment