WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Israel
waje nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo.
Ametoa
kauli jana (Jumatano, Aprili 5, 2017) alipokutana na Balozi wa Israel
nchini Tanzania, Mheshimiwa Yahel Vilan, Ofisini kwake Bungeni mjini
Dodoma.
Waziri
Mkuu amesema Tanzania na Israel ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri
kwa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.
Pia
Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa Israel kuitembelea Tanzania kama
watalii kwa sababu kuna fursa nyingi za utalii ukiwemo mlima wa
Kilimanjaro na mbuga nyingi zilizosheheni wanyama.
Kwa
upande wake, Balozi Vilan ameipongeza Serikali kwa utendaji wake,
ambapo amesema viongozi wa makampuni 50 kutoka nchini Israel wanatakuja
nchini mwaka huu kushiriki katika jukwaa la biashara na uchumi kati ya
Tanzania na Israel.
Amesema
mbali na kushiriki katika jukwaa hilo, pia viongozi wa makampuni hayo
watapata fursa ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini.
Pia
Balozi Vilan amesema Serikali ya Israel itaimarisha kitengo cha
wagongwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa
mkoani Dodoma pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho.
No comments:
Post a Comment