Zaidi ya kampuni 40 kutoka Ufaransa zipo nchini kuwekeza kwenye umeme utakaosambazwa vijijini.
Balozi
wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema jana kuwa, kampuni hizo
zimekuja kwa majadiliano na sekta za umma kuhusu namna ya kuwekeza.
Alisema
wanaosimamia uwapo wa kampuni hizo ni Wizara ya Mambo ya Nje na
Maendeleo ya Kimataifa ya Ufaransa chini ya Wakala wa Biashara wa nchi
hiyo na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Wakati
huohuo, Naibu Waziri wa Fedha wa Korea Kusini, Song Eon-Seog amesema
wametoa Dola 88 milioni za Marekani kusaidia uboreshaji wa mazingira kwa
nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.
No comments:
Post a Comment