Vurugu zaibuka kwenye kituo cha kupiga kura cha Mbasa Mlimani (wilayani Ifakara)baada ya wafuasi wa vyama vya siasa kuwania kuvamia kituo hicho ambapo jeshi la Polisi lilizamika kurusha mabomu ya machozi ili kuzibiti hali hiyo.
Inadaiwa kuwa virugu hizo zilitokana na uchgauzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbasa ambapo wafuasi hao walipinga matokeo ya uchaguzi huo na kutaka kuvamia kituo hicho.
Vurugu hizo zilisababisha askari Huruma Mkisi kujeruhiwa kwa kupigwa jiwe kichwani na mfuasi asiyefahamika na hivyo kupelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis ya Ifakara kwa ajili ya matibabu.
Mashabiki hao walianza kwa kulalamikia matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa kutangazwa na hivyo kuwatilia shaka mawakala ambao walikuwa wakibishana kuhusu idadi ya kura walizopata wagombea wao.
Akitangaza matokeo, msimamizi wa Uchaguzi huo Gaston Kaputa alimtaja mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa Kijiji cha Kisawila kuwa ni Shaaban Salahange wa CCM aliyepata kura 557 aliyefuatiwa na Odric Matimbwa (Chadema) aliyepata kura 528 huku mgombea wa NCCR-Mageuzi Bakari Mkungundile akiambulia kura mbili.
No comments:
Post a Comment