Saturday, September 16, 2017



Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee amefunguka na kusema kwa hali ilivyo sasa Tanzania ni wazi kuwa amani haipo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma na kudai hali hiyo inaleta hofu miongoni mwa wananchi.

Lady Jaydee alisema  kitendo cha Mbunge Tundu Lissu pamoja na Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni wazi kuwa amani ya nchi haipo.

"Ni kweli Tanzania hakuna amani kwa sababu kitendo cha mtu kupigwa risasi hadharani inatishia amani ukizingatia kuna wasanii wengine walikuwa wanatekwa unaogopa, sehemu yenye amani vitu kama hivyo haviwezi kutokea, na kitendo cha Meja mstaafu wa JWTZ kupigwa naye risasi inaongeza kabisaa Tanzani kuwa amani haipo naweza kuwa sina la kusema ila nikaishia kusikitika tu" alisema Lady Jaydee

Aidha Lady Jaydee anasema matukio haya yanaotoa picha mbaya kuwa kama nchi tunakokwenda si sehemu nzuri

No comments:

Post a Comment