Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha
za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na
2016/17.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella
Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali
inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo
kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.
Amesema
kuwa katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016
jumla ya shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na
pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi,
2017 jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu
22420.
Aidha
katika malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya
madeni ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu
Korogwe.Akizungumzia upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema
kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha
madaraja kama inavyotakiwa.
Aidha
amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa
ikiwapandisha vyeo watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika
mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao
watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.
Uhakiki
wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na
taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.
No comments:
Post a Comment