Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la
taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya
kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya
kidiplomasia.
Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kuwa mkakati muhimu pia utakuwa kuirai China kuishinikiza Pyongyang.
Seneta mmoja alisema kuwa habari hiyo kuhusu Korea Kaskazini ilikuwa muhimu sana.
Taarifa iliotolewa kwa niaba ya wizara ya Ulinzi na ile ya kigeni
ilisema kuwa Marekani bado itaendelea na mazungumzo lakini imejiandaa
kujitetea pamoja na washirika wake.
Awali kamanda mkuu wa Marekani katika eneo la Pacific alitetea kupelekwa kwa mfumo wa silaha za kisasa nchini Korea Kusini.
Hali ya wasiwasi imepanda huku kukiwa na hofu kwamba Korea Kaskazini inapanga kujaribu makombora mapya.
''Marekani inataka uthabiti na kutoenea kwa silaha za kinyuklia katika
rasi ya Korea'', ilisema taarifa ya pamoja iliotolewa na waziri wa
maswala ya kigeni REx Tillerson, waziri wa Ulinzi Jim Mattis na
Mkurugenzi wa maswala ya ya ujasusi Dan Coats.
No comments:
Post a Comment