Thursday, April 27, 2017

GAMBO AWATAKA WALIOKULA PESA ZAUMA KUFUNGULIWA MASHTAKA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ametaka kurejeshwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Juma Iddi, Mwekahazina Kessy Mpakata pamoja na Dr. Bakari Salum ambao wataungana na Katibu wa Afya Optat Ismail ili kujibu tuhuma zinazowakabili za ubadhirifu wa Fedha  za mfuko wa pamoja wa kapu la Afya (Busket Fund).

Gambo ameyasema hayo katika siku ya kwanza ya ziara yake Jijini hapa ambapo alikuatana na wafanyakzi wa Jiji, Taasisis za Serikali, Bodi na Kamati za Shule, Viongozi wa Dini, Wazee wa Mji pamoja na Makundi Maalum.

Alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kupokea Taarifa ya Tume aliyoiunda kukagua matumizi ya mfuko huo wa Afya endapo taratibu zilizingatiwa katika mapato na matumizi na kama Fedha hizo ziliwafikia wananchi kupitia huduma bora za Afya.

Aliongeza kusema kuwa kupitia Taarifa ya Tume hiyo alibaini ubadhirifu wa Fedha hizo kwani  zilipelekwa kwenye Hospital ya St. Elizabert pamoja na Isnasheer pasipo kuwa na Mikataba inayoeleweka na mikataba mingine kutokuonekana kabisa hivyo kuwa na mashaka na matumzi ya Fedha hizo na manunuzi ya madawa kufanyika pasipo kuwa na risit za kielektroniki.

“Alisema kuwa haiwezekana Fedha zitumiwe kana kwamba hakuna miongozo wala maelekezo ya Serikali kwa sababu Hospital zingine zimekwisha fungwa lakini bado inaonekana Fedha zilipelekwa sasa sijui zilikuwa zinatumiwa kwenye eneo gani wakati Hospital Haifanyi Kazi”
Rc Gambo pia alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia kuwasimamisha Kazi watumishi 23 wa Timu ya Menegimet ya Afya(CHMT) kupisha uchunguzi wa matumizi ya Tsh Mil 63 walizojilipa posho pasipo kuwa na Taarifa ya kazi(Activity report).

Ziara hii za siku tabo itahusisha uzinduzi na uwekaji na ufunguaji wa miradi ya maendeleo, mikutano ya hadahara pamoja na kutatua kero za wananchi wa Jiji hili.

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.

No comments:

Post a Comment