Tuesday, March 7, 2017

WAZIRI MBARAWA AIASA TEMESA


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kushiriki kikamilifu shughuli za matengenezo ya vivuko ili kupata ujuzi wa ufungaji wa mifumo kutoka Kampuni zinazotengeneza vivuko vya Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuvko kipya cha MV Kazi, Bandarini jijini Dar es Salaam leo, Waziri Profesa Mbarawa amesema  kuwa kupitia mafunzo hayo Serikali itaweza  kuokoa fedha nyingi ambazo kwa sasa inatumia kulipa kampuni binafsi  zinazojenga na kukarabati vivuko

“Hakikisheni mnapata ujuzi kama walionao hawa, hatutaki kutumia fedha za Serikali kwa ajili ya kukarabati au kutengeneza vivuko wakati nyinyi TEMESA mpo”, amesema Waziri Profesa Mbarawa

Pamoja na ujenzi wa kivuko hicho Waziri Mbarawa amewataka Temesa kuhakikisha wanasimamia na kukitunza kivuko hicho ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment