Wednesday, March 22, 2017

WAASI WASHAMBULIA TENA DAMASCUS

Vikosi vya waasi na wapiganaji wa Jihad nchini Syria vimesema kuwa shambulio la hivi karibuni walilotekeleza mjini Damascus, kubwa zaidi kutokea katika kipindi cha miaka miwili ,linapeleka ujumbe kwa serikali siku kadhaa kabla ya awamu nyingine ya mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kuanza mjini Geneva.

Wapiganaji wamesema shambulio hilo lililotokea umbali wa chini ya kilometa tatu kutoka mji wa kihistoria Damascus, unaonyesha kuwa bado wana uwezo wa kufanya shambulizi kubwa katika mji ambao unaelezwa kuwa na ulinzi mkali.

Kuhusu mkutano huo mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amesema pande zote zimethibitisha kuwa zitashiriki kwenye mazungumzo hayo

No comments:

Post a Comment