Maombi
ya mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji dhidi Idara ya Uhamiaji
yamechukua sura mpya baada ya Serikali kutakiwa iwasilishe kiapo kinzani
za majibu.
Mahakama imeagiza Serikali ifanye hivyo ifakapo Jumatatu ijayo na imepanga kusikiliza maombi hayo siku hiyo.
Manji
amefungua maombi hayo katika Mahakama Kuu akihoji uhalali wa
kushikiliwa na idara hiyo huku akiwa bado amelazwa katika Hospitali ya
Aga Khan, jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Uhamiaji inamtuhumu mfanyabiashara huyo kuwa siyo raia wa Tanzania.
Agizo
dhidi ya Serikali la kuwasilisha hati ya kiapo kinzani ikiwa ni majibu
limetolewa na Jaji Ama-Isario Munisi anayesikiliza maombi hayo.
Katika
maombi hayo aliyoyafungua kupitia Wakili wake, Hudson Ndusyepo, Manji
anaiomba Mahakama Kuu iiagize Uhamiaji imfikishe mahakamani ili iamue
uhalali wa kushikiliwa kwake na kisha iamuru aachiwe huru.
No comments:
Post a Comment