Uchaguzi
wa Wajumbe Tisa (9) watakaoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) unatarajiwa kufanyika katika
Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza Aprili 4 mwaka huu.
Uchaguzi
huo utakaofanyika Dodoma, utazingatia maisha ya bunge hilo lililoingia
madarakani mwaka 2012 ambalo litafikia ukomo wake Juni 4 mwaka huu.
Taarifa
iliyoletwa kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Bunge cha Habari, Elimu
na Mawasiliano imeeleza kuwa uchaguzi huo utasimamiwa na Katibu wa
Bunge ambaye atatoa tangazo kwenye gazeti la serikali la leo.
“Katibu
wa Bunge atatoa tangazo kwenye Gazeti la Serikali kesho( leo ) tarehe
17 Machi, 2017 linaloainisha siku ya uteuzi wa wagombea kuwa tarehe 30
Machi, 2017 saa kumi kamili jioni na siku ya uchaguzi kuwa ni tarehe 4
Aprili, 2017 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni.”
Ilisema taarifa hiyo
Katika taarifa hiyo, msimamizi wa uchaguzi alitoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kugombea na kuchaguliwa wajitokeze.
No comments:
Post a Comment