Baada
ya msanii Harmorapa kupata Ubalozi wa kinywaji kinachoitwa cider
‘swala’, Mwanasheria maarufu Alberto Msando ambaye amekuwa
akizishughulikia kesi za wasanii maarufu kama Wema Sepetu na wengineo,
ametoa pongezi kwa msanii huyo.
Msando
ametoa pongezi hizo kwa Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram
akimpongeza kwa hatua aliyopiga na kujitahidi kutengeneza umaarufu ambao
wengi wameshindwa.
"I
really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha
kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na
kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi
hawawezi.
"Wengi
wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu.
Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider ‘swala’. Its a big
step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake
namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby ππππ
"Kisa
tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa
kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza
kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama
wengine. #TheDon#HarmoMbio
#HarmoBastola#KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa
ππ#NusuUsoNusuPua"
No comments:
Post a Comment