"Baada ya kupokea maelezo ya Tanesco na kufuatia tamko la Rais, Jeshi la Wananchi limetafakari na limefanya jitihada kupata fedha za kupunguza deni hili, tunadaiwa fedha kiasi kinachozidi kidogo Sh3 bilioni na Tanesco peke yake, tayari nimeagiza watendaji wetu watafute kiasi cha Sh 1 bilioni na wahakikishe kesho Marchi 27, cheki inawafikia Tanesco haraka ili huduma hiyo iendelee kutumiwa." Alisema Mabeyo.
Pamoja na hayo Mkuu huyo amesema ufinyu wa bajeti umekuwa changamoto kubwa kwao katika kukabiri mahitaji makubwa katika jeshi hilo.
Kwa upande mwingine Mabeyo ameshauri na kusisitizia kwa Taasisi nyingine za Serikali kulipa deni ili kuongezea Tanesco uwezo wa kutoa huduma bora zaidi sekata za utumishi pamoja na kwa wananchi kwa ujumla ambao mpaka sasa wanashida ya umeme.
No comments:
Post a Comment