Kama
umekonda na kudhoofika mwili kutokana na sababu mbalimbali
kama vile kuugua magonjwa na maradhi mbalimbali au kupatwa na
msongo mawazo, basi fuata maelekezo yafuatayo ili upate kujua
namna ya kuandaa na kutayarishe lishe maalumu ya asili itakayo
kusaidia kunenepa na kurejesha afya ya mwili wako katika hali
yake ya kawaida.
MAHITAJI:
1. Dawa Lishe ya kuongeza na kunenepesha mwili
2. Asali ya tende
3. Ufuta
4. Ukwaju
5. Kitunguu swaumu
6. Giligiliani
7. Juisi ya Komamanga na Asali
MATAYARISHO NA MATUMIZI
Matumizi
ya lishe hii, yame gawanyika katika awamu kuu mbili. Awamu ya
kwanza, itachukua siku thelathini na awamu ya pili itachukua
siku thelathini pia.
Katika
awamu ya kwanza , mgonjwa atatumia DAWA LISHE YA KUNENEPESHA
MWILI, ASALI YA TENDE NA UFUTA na awamu ya pili, mgonjwa
atatumia UKWAJU, KITUNGUU SWAUMU, GILIGILIANI na JUISI YA
KOMAMANGA & ASALI kwa kufuata utaratibu utakao elezwa hapo
chini.
AWAMU YA KWANZA
SIKU THELATHINI ZA KWANZA
Mahitaji
1. Dawa lishe ya kuongeza na kunenepesha mwili
2. Ufuta
3. Asali ya Tende ( Dates Syrup )
MATAYARISHO , MAELEKEZO NA MATUMIZI
1. Dawa –Lishe ya Kunenepesha Mwili
Chukua
vijiko vitatu vikubwa vyenye dawa yako, kisha changanya na
maji nusu lita halafu chemsha hadi itokote, Ikiisha tokota, ipua
acha ipoe kidogo kisha tumia kunywa pamoja na machicha yake.
Utafanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda
wa siku thelathini.
2.
Ufuta : Matayarisho : Chukua vijiko vikubwa vinane vyenye ufuta,
kisha changanya na lita moja na nusu ya maji. Kama hauna
tatizo na sukari, unaweza kuongeza na sukari kiasi ili kuipa
ladha. Ikisha tokota, ipua iache ipoe kiasi kisha tumia kula
ufuta wote pamoja na supu yake ama juisi yake. Utafanya hivyo
mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku
thelathini.
(N.B:
KAMA UNA NAFASI, BADALA YA KUTUMIA VIJIKO VINANE TU VYA UFUTA
KWENYE LITA MOJA NA NUSU YA MAJI, WEWE TUMIA ROBO KILO YA
UFUTA KWENYE LITA TATU YA MAJI, CHEMSHA HADI ITOKOTE, IACHE
IPOE, KISHA TUMIA KULA . FANYA HIVYO MARA MBILI KWA SIKU ASUBUHI
NA JIONI KWA MUDA WA SIKU THELATHINI )
2. ASALI YA TENDE
3.
Tumia kula vijiko vikubwa vinne vya tende mara mbili kwa siku
asubuhi na usiku kwa muda wa siku thelathini. Yaani asubuhi
kula vijiko vikubwa vinne na usiku kula vijiko vikubwa vinne
vya asali ya tende.
(
HABARI NJEMA KWA WATEJA WETU NI KWAMBA, ASALI YA TENDE SASA
INAPATIKANA MOJA KWA MOJA DUKANI KWETU . UTAPATIWA DAWA LISHE
PAMOJA NA ASALI YA TENDE UTAKAYO ITUMIA KWA MUDA WA SIKU
THELATHINI KWA UTARATIBU WA MAELEKEZO HAYO HAPO JUU )
AWAMU YA PILI
Awamu
ya pili ya lishe hii, itaanza baada ya kukamilika kwa siku
thelathini za kutumia dawa lishe, ufuta pamoja na asali ya
tende. Kama ilivyo kuwa kwa awamu ya kwanza, awamu ya pili pia
itachukua muda wa siku thelathini
MAHITAJI, MATAYARISHO NA MATUMIZI
1. UKWAJU
Matayarisho na Maandalizi
Chukua
ukwaju kiasi cha robo kilo , weka kwenye maji kiasi cha lita
moja, ongeza pilipili manga kiasi cha kijiko kimoja kidogo ( tea
spoon ) halafu ongeza sukari vijiko vitatu vikubwa, ongeza karafuu ya
unga kijiko kimoja kidogo, pamoja na hiriki vijiko vikubwa viwili.
Ukisha
fanya hivyo, chemsha hadi mchanganyiko wako utokote. Ukisha
tokota, ipua na kuchuja kisha weka kwenye chombo kisafi.
MATUMIZI :
Tumia
kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi baada ya kunywa chai.
Utafanya hivyo kwa muda wa siku thelathini mfululizo.
2. JUISI YA KOMAMANGA NA ASALI
Matayarisho na Matumizi
Tayarisha
juisi ya komamanga kiasi cha nusu lita, changanya na asali ya
kawaida vijiko vikubwa vinane, kisha ongeza chumvi kijiko kidogo(
tea spoon)
Koroga mchanganyiko wako halafu tumia kunywa. Utafanya hivyo mara moja kwa siku kwa muda wa siku thelathini.
Matunda
ya makomamanga yanapatikana masokoni, ingawa mara nyingi
hupatikana kwa uchache. Kama utabahatika kupata matunda mengi,
basi unashauriwa kuyachukua kwa wingi na kuyahifadhi, sehemu
salama ili usipate usumbufu wakati wa kutumia tiba yako.
Mbali
na kutumika katika lishe ya kuongeza na kunenepesha mwili,
tunda la komamanga, linasaidia kuondoa harufu mbaya ya kinywa.
Kwa kuondoa harufu mbaya ya kinywa, kula walau tunda moja la
komamanga kwa siku kwa muda wa siku thelathini mfululizo.
Utapata matokeo mazuri . ( HII ITAWASAIDIA ZAIDI WALE AMBAO
TATIZO LAO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA YA KINYWA LIMEANZIA
KINYWANI NA SIO TUMBONI
ALTERNATIVE (MBADALA ) WA JUISI YA KOMAMANGA ILIYO UNGWA NA ASALI.
Kama utashindwa kupata makoma manga, basi utafanya kama ifuatavyo :
KITUNGUU SWAUMU
Chukua
punje nne za vitunguu swaumu, zitwange kisha tia kwenye maji
nusu lita halafu ongeza juisi ya ndimu moja au limao moja kisha
chemsha hadi mchanganyiko wako uchemke.
Matumizi
: Tumia hivyo kila siku usiku baada ya kula chakula cha usiku.
Utafanya hivyo kwa muda wa siku thelathini mfululizo.
AU
Vile
vile , mbadala mwingine wa kutumia juisi ya komamanga iliyo
changanywa na asali, unaweza kutumia JUISI YA GILIGILIANI kwa
kufuata utaratibu ufuatao :
JUISI YA GILIGILIANI
MATAYARISHO NA MATUMIZI YA JUISI YA GILI GILIANI
Chukua giligiliani fresh, kisha zi -blend ( ZISAGE ) ili kupata juice yake kiasi cha robo lita.
Ndani
ya juisi yako ya giligiliani, kamuliamo ndimu fresh moja, halafu
ongeza chumvi kiasi robo kijiko kidogo ( tea spoon), koroga kisha
tumia kunywa. Utakunywa usiku baada ya kula chakula cha usiku.
Utafanya hivyo mara moja kwa siku kwa muda wa siku thelathini
mfululizo.
PIA
: Jenga utaratibu wa kuwa unakula giligiliani kwa wingi.
Hakikisha katika kila mlo wako, inakuwepo mboga ya giligiliani
pembeni.
VITU VINGINE VYA KUZINGATIA..
Pamoja
na kutumia lishe hii ya asili kwa kufuata utaratibu huo hapo
juu, unashauriwa kuzingatia matumizi ya vyakula vifuatavyo:
TANGAWIZI
Jenga
tabia ya kuwa una tumia tangawizi, kila mara upatapo nafasi.
Utaratibu wa jinsi ya kutayarisha tangawizi ni kama ifuatavyo :
Chukua
kipande kimoja cha tangawizi, kisha kitwange halafu ongeza
vikombe viwili vya maji vyenye ujazo wa milimita mia mbili na
hamsini ( 250 mills). Chemsha pamoja kisha ongeza maziwa kiasi cha
robo lita na sukari ili kupata ladha. Fanya hivi kila mara
uapatapo nafasi. Ukiweza kufanya hivyo walau mara mbili kwa siku,
itakuwa vizuri zaidi.
AU chukua kipande kimoja cha tangawizi, kitwange kisha chemsha
pamoja na chumvi nusu kijiko kidogo kwenye maji kiasi cha nusu
lita halafu tumia kunywa kikombe kimoja nusu saa kabla ya
kula chakula chako cha asubuhi, mchana na usiku.
HIRIKI
Jenga utaratibu wa kuwa unakunywa mara kwa mara chai iliyo changanywa na hiriki.
MACHUNGWA
Jenga
utaratibu wa kuwa unakula machungwa kwa wingi, kwa kadri
utakavyo weza. Unashauriwa kuwa unachanganya na chumvi kidogo
pamoja na pilipili manga.
KWA MAHITAJI YAKO YA DAWA-LISHE YA KUNENEPESHA & KUONGEZA MWILI PAMOJA NA ASALI YA TENDE.
Kwa
mahitaji yako ya DAWA-LISHE ya kuongeza & kunenepesha mwili,
pamoja na asali ya tende, fika katika duka la NEEMA HERBALIST.
Tunapatikana
UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI
UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA.
WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0766 53 83 84.
Kwa
wateja wetu waliopo jijini Dar Es Salaam, ambao hawana nafasi
ya kufika dukani kwetu Ubungo, tunayo huduma ya kuwapelekea
dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY )
Kwa wateja waliopo nje ya mkoa wa Dar Es Salaam, watatumiwa dawa kwa kutumia mabasi mbalimbali.
Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.
Kwa wateja waliopo ughaibuni, watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.
No comments:
Post a Comment