GEORGE LWANDAMINA.
Droo hiyo ya kupanga ratiba hiyo itafanyika leo saa 5:00 asubuhi kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) yaliyoko jijini Cairo, Misri.
Mechi ya kwanza ya hatua hiyo ya mtoano kabla ya kuingia makundi imepangwa kufanyika kati ya Aprili 7 na 9 huku ile ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa kati ya Aprili 14-16, mwaka huu.
Mbali na Yanga, timu nyingine zitakazohusika katika droo hiyo ni pamoja na RC Kadiogo ya Burkina Faso, AC Leopards (Congo), AS Tanda (Ivory Coast), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Gambia Ports Authority (Gambia), Horoya (Guinea), CNaPS (Madagascar), AS Port Louis (Mauritius), FUS Rabat, Wydad Athletic Club (Morocco), Ferroviario Beira (Msumbiji), Rivers United, Rangers (Nigeria), Bidvest (Afrika Kusini) na KCCA ya Uganda.
Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema jana kuwa mazoezi ya timu hiyo yatasimamiwa na Kocha Msaidizi, Juma
Mwambusi kutokana na Kocha Mkuu, George Lwandamina kubaki kwao Zambia, na wanaamini baadhi ya nyota waliokuwa wagonjwa watarejea uwanjani wiki hii.
Aliongeza kuwa Lwandamina anatarajiwa kurejea nchini kesho kuendelea na majukumu yake .
Mkwasa alisema kuwa benchi la ufundi limeshayaangalia makosa waliyofanya katika mechi mbili za kimataifa zilizopita ili kusahihisha na hatimaye kufanya vizuri kwenye mchezo wao unaofuata.
"Mazoezi yatakuwa ni ya kawaida kwa siku tatu za kwanza kwa sababu baadhi ya wachezaji wanatakiwa kuripoti kwenye kambi ya Stars (Timu ya Taifa), watakaobakia watakuwa chini ya Mwambusi," alisema Mkwasa.
Yanga imehamia katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia sare ya bao 1-1 waliyopata katika mechi ya kwanza huku mabingwa hao watetezi wa Bara wakilazimishwa suluhu ugenini, hivyo Wazambia hao kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
No comments:
Post a Comment