Kampuni ya simu za mkononi inatarajia kumwaga mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuidhamini klabu ya Yanga.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza, Mwenyekiti wao, Yusuf Manji
tayari aliwaeleza baadhi ya watendaji wake nia ya namna ambavyo Yanga
inaweza kufaidika na udhamini mkubwa wa zaidi ya Sh bilioni 4.
“Mwenyekiti
alikuwa na mpango huo, alishazungumzia suala hilo hapo awali. Lakini
kumekuwa na mambo kadhaa yaliyotakiwa kumalizia.
“Hata
sisi mwanzo hatukujua ni Tigo kwa kuwa hakuwa ameeleza kama ni kampuni
gani ya simu. Lakini baadaye tuligundua ni Tigo,” alieleza mmoja wa
viongozi ndani ya Yanga.
“Lengo
lake ni Yanga kuwa kubwa Afrika na bila udhamini ni sawa na
kujidanganya. Hivyo kama mmiliki wa Tigo, ni rahisi Yanga kupata
udhamini huo ingawa ninaamini kama kampuni ingedhamini hata timu
nyingine.
“Kwa
sasa, labda tusubiri misukosuko ipungue ndiyo mwenyewe anaweza
kuzungumza. Maana sasa yuko Hospitali, mara mahakamani hivyo hajatulia.”
Manji kwa sasa analezwa kuwa mmiliki halali wa Tigo baada ya kuinunua katika mnada mwaka 2014 mwishoni.
Lakini kuna kesi imefunguliwa ya kuanzisha upya mnada wa ununuzi wa kampuni hiyo ukidaiwa kuwa una walakini.
No comments:
Post a Comment