Agness Gerald (25) maarufu kama Masogange na wafanyakazi 14 wa kampuni ya Quality Group wameshafikishwa mahakama ya Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka kuhusu tuhuma za madawa ya kulevya. Leo tarehe 22 february
Masogange
alitarajiwa kupandishwa kizimbani Ijumaa wiki iliyopita lakini
ilishindikana kutokana na majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali dhidi ya
vipimo vyake kuonesha kama anatumia au hatumii dawa hizo kutokamilika.
Hata
hivyo alitarajiwa kufikishwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi
ambapo alikwama tena kutokana na jalada lake kupelekwa kwa AG.
Wakili
wa Masogange, Nick Kitege amesema bado jalada la Masogange lipo kwa AG
na anaendelea kulifanyia kazi na pindi litakapokamilika muda wowote
anaweza kupelekwa mahakamani.
Alisema jalada hilo limechelewa kutokana na taratibu za kisheria zinazofanywa ili kukamilisha uchunguzi.
“Bado
tupo tunafuatilia na jalada la kesi yake kwa sasa lipo kwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali pindi taratibu zitakapokamilika atafikishwa mahakamani
kati ya leo au kesho.
“Kuhusu
ucheleweshwaji wa kesi hiyo ni kutokana na taratibu za kisheria, hivyo
Polisi waachwe wafanye kazi yao na sisi tunaangalia hatua
zinazoendelea.
“Unajua
hivi ni vyombo vya sheria na wanafanya kazi yao, wanahitaji muda
kuchunguza na kutoa hoja zilizojitosheleza, bado wanahangaika
kushughulikia suala hilo naamini leo tutapata jibu kamili,” alisema Kitege.
Julai
mwaka 2013 Masogange alikamatwa Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Oliver Tambo, akiwa na mwenzake aliyejulikana kwa jina la
Melisa Edward wakiwa na mzigo wa dawa za kulevya wenye thamani ya zaidi
ya Sh bilioni 6.8.
No comments:
Post a Comment