Rais wa Gambia Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie.
Jenerali Badjie alitangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani
Yahya Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute.
Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi
vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi
jana.
Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.
No comments:
Post a Comment