Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana
Tarehe 31 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Marais watatu
wa Nchi za Afrika, Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kando ya Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi
Wanachama wa Umoja wa Afrika uliomalizika leo Mjini Addis Ababa Nchini
Ethiopia.
Mhe.
Rais Magufuli amewaalika viongozi wote kuitembelea Tanzania ili wapate
muda zaidi wa mazungumzo ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kwa lengo
kukuza zaidi biashara, uwekezaji na kuboresha maisha ya wananchi.
Kwanza,
Mhe. Rais Magufuli amekutana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri
Kaguta Museveni ambapo viongozi hao wamezungumzia miradi mbalimbali ya
ushirikiano na fursa za biashara ambazo Tanzania na Uganda zinaweza
kuzitumia kujiongezea mapato. Mhe. Rais Museven amekubali kufanya ziara
nchini Tanzania katika siku za karibuni.
Pili, Mhe
Rais Magufuli amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe.
Abdel Fattah El-Sisi ambapo viongozi hao wamezungumzia namna nchi hizo
zitakavyoshirikiana katika nyanja mbalimbali zikiwemo afya, kilimo,
mifugo na viwanda.
Pamoja
na kukubali mwaliko wa Rais Magufuli wa kufanya ziara rasmi nchini
Tanzania, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi pia amekubali ombi la kuwaleta
wataalamu na wawekezaji wa Misri nchini Tanzania ili wajenge viwanda vya
kuzalisha dawa na vifaa tiba vya binadamu, kuinua teknolojia ya kilimo
cha umwagiliaji, kuwekeza katika viwanda vya nyama na viwanda vingine
ambavyo nchi hiyo imepiga hatua kubwa.
“Mhe.
Rais El-Sisi nakupongeza sana kwa juhudi zako za kuijenga Misri na
nitafurahi sana kuona biashara ya Tanzania na Misri inaongezeka maradufu
kwa manufaa ya pande zote mbili” amesisitiza Mhe. Dkt Magufuli.
Tatu, Mhe.
Rais Magufuli amekutana na Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma
ambapo pamoja na kukubali kufanya ziara rasmi nchini Tanzania, viongozi
hao wamekubaliana kuwa baada ya kazi kubwa ya harakati za ukombozi nchi
hizi sasa zina kila sababu ya kuelekeza nguvu katika kuongeza biashara
na uwekezeji.
Nne,
Mhe. Rais Magufuli amekutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) Bw. Akinwumi Adesina ambapo pamoja na kumshukuru kwa ushirikiano
mzuri ambao Tanzania inaupatakutoka Benki hiyo katika utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo, amemuomba kuendeleza na kuongeza zaidi
ushirikiano huo hasa katika maeneo ya kipaumbele ambayo Tanzania
inayatekeleza hivi sasa.
Kwa
upande wake Bw. Akinwumi Adesina amesema Benki hiyoitaendeleza
ushirikiano na uhusiano wake na Tanzania na kwamba Tanzania itanufaika
kupitia vipaumbele vipya vya AfDB viitwavyo “Hi 5” vinavyohusisha
uwezeshaji miradi ya uzalishaji wa nishati, ujenzi wa viwanda,
uzalishaji wa chakula, miundombinu ya kuunganisha nchi na nchi na
kuboresha maisha ya watu.
Pia
Bw. Akinwumi Adesina amekubali ombi la Mhe. Rais Magufuli la kuitaka
AfDB kushirikiana na Tanzania kupata suluhisho la kuzalisha umeme mwingi
na wa gharama nafuu na ameahidi kumtuma Makamu wa Rais wa AfDB
anayeshughulikia masuala ya nishati kuja Tanzania haraka iwezekanavyo
ili kuanza utekelezaji wa ombi hilo.
Tano,
Mhe. Rais Magufuli amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.
Hailemariam Desalegn na amemualika kufanya ziara rasmi nchini Tanzania
ili wapate nafasi ya kuzungumza zaidi juu ya kuimarisha uhusiano na
ushirikiano kati ya nchi hizo.
Pamoja
na kukubali mwaliko wa Rais Magufuli, Mhe. Hailemariam Desalegn
amempongeza kwa mabadiliko makubwa ya uchumi ambayo Serikali ya awamu ya
tano inayafanya nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kukabiliana na
vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Mkutano
wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ambao Rais
Magufuli amehudhuria kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani
umemalizika jana Mjini Addis Ababa na Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa
kurejea nyumbani leo
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Addis Ababa
No comments:
Post a Comment